Vyama vya siasa vya upinzani nchini vimemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kujishusha kufuatia sakata baina ya Bunge na CAG kutokana na kusababisha mgongano baina ya Mamlaka
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa amesema kwa hali ilivyo sasa ya Spika kumtaka CAG kwenda kwa Rais kujieleza ni kuongeza mkanganyiko zaidi unaowaweka Wananchi njia panda juu ya uangalizi wa hesabu za miradi ya maendeleo
Wakati huo huo CHADEMA, CHAUMA, ACT Wazalendo, Democratic Party, CCK na UPDP vimeungana na kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga matumizi ya Sheria ya vyama vya Siasa vinavyodai inakandamiza misingi ya demokrasia
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema katika kesi yao wameomba Mahakama ya Afrika Mashariki kutoa zuio la matumizi ya Sheria hiyo mpaka kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo