Vyama vya upinzani vyaungana kumng'oa madarakani Rais Museveni 2021

Vyama vitatu vya upinzani nchini Uganda vimetia saini mkataba wa ushirikiano kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao, vikiwa na lengo la kumpata mgombea mmoja kupambana na rais Yoweri Museveni.

Vyama hivyo vilivyotia saini mkataba huo ni pamoja na kile cha DP, kinachoongozwa na Nobert Mao, chama cha People`s Progressive party na chama cha Social Democratic party.

“Sasa tumeungana kwa ushirikiano ikiwa ni pamoja na Alliance for National Transformation, Robert Kyagulanyi (Bobiwine)na people power. Tutakuwa na mgombea mmoja ambae atapeperusha bendera yetu”, amesema Nobert Mao, mmoja wa makada wa chama kimoja cha upinzani kilichoshiriki muungano huo.

Hatua hiyo imesifiwa na Bobi Wine, mwanasiasa kijana nchini Uganda ambaye amepata umaarufu hivi karibuni, huku akibaini kwamba muungano huo wa wapinzani ni tishio kwa rais Museveni.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa muungano huu utakuwa na nguvu zaidi iwapo chama kikuu cha upinzani FDC kitaungana na wengine kuongeza nguvu kutokana na umaarufu wa Kiiza Besigye. Hii ni mara ya tatu kwa vyama vya upinzani kuungana kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mwaka 2016, kuliundwa muungano uliofahamika kama Democratic Alliance, lakini haukufaulu kuingia Ikulu ya Entebee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad