Waandamanaji Katika Makao Makuu ya Jeshi Waongeza Shinikizo Dhidi ya Dais Omar al-Bashir Ajiuzulu

Maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan, wakimtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu.

Inavyoonekana wanatarajia mapinduzi ya ndani ya nchi, wakiliomba jeshi kumtimua Bashir na kufungua njia ya kupatikana serikali ya mpito.

Ni maandamano makubwa dhidi ya Bashir tangu kuzuka ghasia mnamo Desemba mwaka jana.

Mauaji ya Kimbari:Yatima watafuta familia zao
Jangili auawa na Tembo kisha aliwa na Simba
Ulimwengu wenye wazee wengi kuliko watoto
Bashir amekataa kuondoka, akieleza kwamba wapinzani wake wanastahili kutafuta uongozi kupitia uchaguzi. Jeshi halijaingilia kati.

Maafisa wa usalama wamefyetua gesi ya kutoa machozi kuwatimua wandamanaji nje ya makao hayo makuu katika mji mkuu, Khartoum.

Waandamanaji walipiga kelele "jeshi moja, watu wamoja" nje ya makao mkauu ya jeshi Sudan
Maandamano haya yanaadhimisha miaka 34 ya mapinduzi yaliouondoa utawala wa rais Jaafar Nimeiri.

Katika maandamano ya nyuma, wamettumia pia guruneti na silaha za moto zikiwemo risasi. waandamanaji kadhaa wameuawa .

Siku ya Jumamosi, mwandamanaji mmoja alifariki katika mji wa Omdurman, polisi wanasema.

Waziri wa habari nchini Sudan amethibitisha mipnago ya serikali kutatua mzozo kupitia mazungumzo na kupongeza vikosi vya usalama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad