Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mji wa Tarime mkoani Mara wamamelazimika kuanika wadaiwa sugu wa bili ya Ankara za maji Machi,2019 na kuwataka kulipa haraka kwa mjibu wa taratibu za nchi.
Akiongea kwenye kikao cha Bodi ya mamlaka ya maji kilichofanyika jana kaimu Meneja,Passian Martin alisema kuwa mamlaka inadai Taasisi mbalimbali Ankara za maji zaidi ya shilingi 13,092625.50 machi,2019.
Martin alizitaja Taasisi hizo kuwa ni pamoja na Chuo cha uwalimu Tarime(Tarime Teachers Colleg) TTCshilingi 1046005.00,TMO Hospital 4178431.00Tarime sekondari shilingi 148874.00,27KJ House 204300.00,27KJ shilingi 100635.00,Magereza Shilingi 5311131.00,RPC Tarime Rorya,shilingi 69574.00,Shule ya mazoezi Buhemba shilingi 80175.00,RPC Tarime polisi Line shilingi 436017.00,RPC Tarime Canteen 660734.00,RPC Kikosi cha Mbwa shilingi 316671.50.
wengine ni Chuo cha manesi Tarime NTC Tarime shilingi 228078.00,Bomani Sekondari shilingi 210000.00,TTC Resti House shilingi 102000.00.
Kaimu meneja alisema kuwa kutolipa Ankara za maji kwa wakati ni moja ya kosa la kisheri na pia makusanyo yanashuka na kusababisha shughuli za uendeshaji unakuwa mgumu kwa kuzingatia kuwa shughuli zote zinahitaji fedha ya uendeshaji.
Martin aliongeza kuwa mamlaka ya maji inajiendesha kwa kuzingatia uwezo halisi wa kukusanya Ankara za madeni mbalimbali pamoja na huduma za kiufundi kwa wateja wapya.
Katika kikao hicho mganga mkuu wa hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Mji wa Tarime,Kelveni Mwosha alisema kuwa ndani ya wiki hii atalipa madeni yanayo mkabili ikiwemo deni la hospitali ya Bomani na Chuo cha manesi NTC.