Wagonjwa 250 Walioshindwa Kulipa Gharama za Matibabu Waachiliwa Kenya

Wagonjwa 250 Walioshindwa Kulipa Gharama za Matibabu Waachiliwa Kenya
Hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya imesema kuwa imewaachilia huru wagonjwa 52 kwenda nyumbani kufuatia madai kwamba walikuwa wanazuiliwa baada ya kushindwa kulipa gharama zao za matibabu.

Taarifa kutoka hospitali hiyo ya kitaifa imesema kuwa zaidi ya wagonjwa 250 wameruhusiwa kuondoka.

Hospitali hiyo imekana madai kwamba baadhi ya wagonjwa walikuwa wamezuiliwa kinyume na matakwa yao ijapokuwa duru zinaarifu kuwa ni kawaida kwa hopsitali nchini Kenya kuwazuilia wagonjwa kuondoka hadi wanapolipa gharama zao za matibabu.

Uchunguzi wa hivi majuzi uliofanywa na runinga ya habari ya The Citizen nchini Kenya ulifichua swala hilo na kubaini kwamba baadhi ya wale waliokuwa wakizuiliwa katika hospitali hiyo ni wanawake ambao wamekumbwa na matatizo baada ya kujifungua.

Lakini hospitali hiyo inasema kwamba iliwaachilia huru wagonjwa 258 katika kipindi cha wiki mbili, ikiwemo 52 ambao waliwachiliwa siku ya Jumanne.

Msemaji wa Hospitali hiyo Hezekile Gikambi Peter amekana kwamba wagonjwa hao walikuwa wakizuiliwa na kuongezea kuwa wasingezuiliwa kuondoka katika hospitali.

Anasema kuwa raia hao waliachiliwa baada ya kukubali kulipa gharama za matibabu baada ya kurudi katika biashara zao za kawaida.


Kati ya asilimia 70 iliosalia asilimia 30 huonekana kama wagonjwa wasioweza kulipa gharama zao kwa mfano watoto wa mitaani wasio na familia.
Anasema kuwa wagonjwa hao ni kundi la pili kuachiliwa huru tangu mfumo wa kulipa kwa makubaliano ulipoanzishwa mapema mwezi Machi.

Anasema kuwa baada ya mtu kuachiliwa huru na daktari, anafuzu kuondoka hospitalini -iwapo hawawezi kulipa wanatakiwa kusubiri uchunguzi kufanywa kwa makubaliano ya kulipa.

''Hatua hiyo huchukua kati ya siku 2-3. Wengine hulazimika kusubiri kwa muda mrefu kama wiki moja hivi-kwa kuwa wanawasubiri ndugu zao kuja hospitalini''.

Idadi ya wagonjwa wanaoshindwa kulipa gharama zao
Takriban asilimia 30 ya wagonjwa wanaweza kulipa gharama zao kupitia pesa ama bima na wao huondoka mara tu wanapomaliza kupatiwa matibabu.

Kati ya asilimia 70 iliosalia asilimia 30 huonekana kama wagonjwa wasioweza kulipa gharama zao kwa mfano watoto wa mitaani wasio na familia.

Gharama yao huondolewa na huondoka hospitalini mara tu wanaporuhusiwa kuondoka.

Ni watu wanaosalia hospitalini hata baada ya kuruhusiwa kuondoka wakati wanaposubiri kutia saini makubaliano ya kulipa gharama zao.

Makubaliano mengine yanawaruhusu wagojwa kulipa kidogokidogo kama dola 5 kwa mwezi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad