Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushtakiwa, Wanasheria wajitoa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kapteni mstaafu George Mkuchika, amesema wakuu wa mikoa na wilaya watakaowaweka watu ndani kinyume cha sheria, watashtakiwa wao binafsi, na hawatatetewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


Akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020 , Mkuchika amefafanua kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapotumia mamlaka yao kumuweka mtu mahabusu saa 24 na 48 wazingatie sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

Kapteni Mkuchika amesema viongozi hao wakitekeleza hatua kinyume na utaratibu wanaweza kuchukuliwa hatua ikiwamo kushtakiwa wao binafsi.

"Tumekemea sana hili jambo, sasa hivi mwanasheria wa serikali hatomtetea mtu aliyevunja sheria makusudi kwa kumuweka mtu ndani bila sababu. Utapelekwa mahakamani na huyo uliyemuweka ndani na mwanasheria hatokuja kukutetea,” amesisitiza.

Ameongeza, “Namshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa waraka kwa wote waliopewa mamlaka ya kuweka mtu ndani na mimi kanipa nakala, ikieleza mazingira ya mtu kuwekwa ndani,” alisema Mkuchika jana bungeni.

Amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kuwa na taarifa za maandishi kwanini ameweka mtu ndani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad