Walevi Kukamatwa Uganda Sheria Yatungwa

Polisi nchini Uganda inapania kuzindua mpango wa kuwakamata watembea kwa miguu watakaopatikana wakiwa walevi.

Akitetea mpango huo mpya kamanda wa trafiki katika jiji la Kampala Lawrence Niwabiine amesema kikosi cha polisi hakitaruhusu watu "wahatarishe"maisha yao.

Tayari vyombo vya habari nchini Uganda vimezua gumzo miandaoni baada ya kuangazia mpango huo tata katika mitandao ya kijamii.

'Hali ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa' Msumbiji
Wamuoza binti yao wa 'miaka mitano' kwa dola 3,500
Mwanamitindo afariki akifanya 'catwalk'
Watu wamekua wakihoji jinsi sheria hiyo itakavyotekelezwa hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu wanaokamatwa kila uchao wakiendesha magari wakiwa walevi huishia kuachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivyo mamia ya watu waliyopatikana na hatia ya kuendesha magari wakiwa walevi wameshindwa kulipa faini.
Kuna wale wanaosema kwa kuwa Afande Niwabiine hatumii kileo huenda maafiasa wake wakawatia mbaroni walevi wanaotembea kwa miguu kando ya barabara.

Wengine wanasema hatua hiyo huenda ikawa na athari kwa uchumi wa nchi.

Wanaharakati wanapendekeza mifumu ya kisheria na kijamii iwekwe sawa kabla ya kuanza kutekeleza sheria hiyo.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
''Kabla ya kuanza mpango huo,magereza yatahitaji kupanuliwa haraka iwezekanavyo kwasababu watembezi wengi walevi hawana uwezo wa kulipa faini la sivyo mahakimu watakuwa na kibarua kigumu katika kutoa hukumu dhidi ya watu hao wakati sheria inasem kila mmoja achukukliwe hatua'' alisema mmoja wao.

Pili anasema wafanyibiashara wa pombe watalazimika kuhamisha biashara zao katika maeneo ya makazi ili kupunguza hofu ya wateja wao kukamatwa.

''Hata polisi akipiga kambi karibu na hapo akisubiri kukukamata hataweza kufanya hivyo manake unaweza kuamua kumpigia mmoja wa jamaa zako nyumbani kukuletea mtu ulale ndani ya baa karibu na kwako'' ,aliongeze

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad