Wambura Amjibu Zahera Kuhusiana na Viporo Vya Simba

Wambura Amjibu Zahera Kuhusiana na Viporo Vya Simba
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amemweleza Kocha wa Yanga, mwinyi Zahera, kutokuwa na hofu juu ya mechi za viporo ambayo Simba wanakabiliwa navyo.

Kauli ya Wambura imekuja mara baada ya Zahera kulalamika kila wakati kuhusiana na ratiba ya Simba hivyo mpaka imepelekea kuwa na mechi nyingi mkononi ambazo hazijachezwa mpaka sasa.

Wambura amesema kuwa sababu ya mechi nyingi kutochezwa ni kutokana na changamoto ya viwanja pamoja na ugumu wa ratiba.

Bosi huyo wa Bodi ya Ligi amesema hamna timu ambayo imeandaliwa kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kama wengine wanavyodai mabadiliko ya ratiba ya Simba ni kutokana na ratiba ngumu iliyokuwa nayo kwenye michuano ya kimataifa.

Simba ikirudi kutoka DR Congo italazimika kucheza mechi nyingi ili wasivurunge kalenda ya msimu Pia Wambura amesema leo watatoa ratiba nzima ya Simba na viporo vyake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad