Wamisri Wapiga Kura kumuongezea Muda wa Uongozi Rais wa tayifa Hilo

Raia nchini Misri wameanza kupiga kura ya maoni asubuhi hii inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.


Kura hiyo iliyopingwa na makundi ya haki za binaadamu, inatazamiwa kuridhia mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yataongeza muhula wa al-Sisi madarakani hadi mwaka 2030.

Mbali ya hilo, kura hiyo pia itampa kiongozi huyo wa kijeshi aliyegeuka kuongoza serikali ya kiraia, nafasi ya kuwania tena kwa miaka sita baadaye, madaraka zaidi juu ya mahakama na nguvu kubwa kwa jeshi kushiriki siasa.

Sisi, mwenye umri wa miaka 64, anashutumiwa kuirejesha Misri kwenye zama za udikteta mkubwa na mbaya zaidi kuliko hata wa Hosni Mubarak, ambaye aliondolewa na wimbi la maandamano ya umma miaka minane iliyopita

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nchi za wajanja wanachukua hatua kuwaongezea muda viongozi wao wanaowaamini. Hapa kwetu inatuchukua muda kuamua hivyo. Wakipiga hatua ya maendeleo haraka tubaki kushangaa.
    AMKENI WATANZANIA!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad