Wanajeshi Waizingira Ikulu ya Rais Omar al-Bashir, Wasema Watatoa Tamko Hivi Punde

Wanajeshi Waizingira Ikulu ya Rais Omar al-Bashir, Wasema Watatoa Tamko Hivi Punde
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa litatoa taarifa muhimu hivi karibuni, hali inayohisiwa kuwa utawala wa Rais Omar al-Bashir huenda ukafikia kikomo hivi karibuni.

Wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais mapema asubuhi ya leo, shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.

Jeshi pia limezingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum.

Magari yaliyosheheni wanajeshi wenye silaha yameegeshwa kwenye barabara zote muhimu na madaraja kwenye mji mkuu, shirika la habari la Reuters linanukuu mashuhuda.

Matangazo ya kawaida ya redio ya serikali yamekatishwa na kwa sasa zinapigwa nyimbo za ukombozi.

Raia wanaimba kwa furaha, "serikali imeangushwa. Tumeshinda," shirika la Reauters linaripoti.

Mwanahabari mmoja maarufu na anayeheshimika nchini Sudan, Yousra Elbagir ameandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali wanakamatwa na wanajeshi, na kuwa uwanja wa ndege jijini Khartoum umefungwa.

Hii leo, kulipangwa kufanyika maandamano ya wafuasi wa Bashir ambao walitaka kuonesha uungaji mkono wao kwa kiongozi huyo lakini kuna ripoti kuwa maandamano hayo yamekatazwa.

Maandamano dhidi ya Bashir yalianza toka mwezi Disemba. Awali maandano yalianza kwa kupinga kupanda kwa bei ya vyakula lakini yamekuwa makubwa na kubadili lengo na kutaka kumng'oa rais madarakani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad