Jumanne usiku, wakati tangazo lilipotoplewa, makundi ya vijana waliingia mitaani wakielekea katikati mwa mji, huku wakiomba.
Vifijo na nderemo vimetawala Jumanne usiku katika miji mbalimbali nchini Algeria baada ya hatuwa hiyo ya kujiuzulu kwa rais Bouteflika ambae amekabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Baraza la kikatiba. Raia wengi wa Algeria wanaamini kwamba hii ni hatuwa ya kwanza ya ushindi na wataendelea na maandamano kuhakikisha jopo zima la Bouteflika linaondoka.
Hatua ya kujiuzulu kwa rais Abdelazizi Bouteflika imekuja baada ya jeshi kutoa msimammo wake na kuomba Mahakam ya Katiba kutekeleza Ibara ya 102 ya Katiba inayozungumzia mchakato wa rais asiyewajibika kwa mamlaka yake.