Wananchi Wa Ihanga’na Mkoani Njombe Walalamika Kukosa Umeme Wa REA

Wananchi Wa Ihanga’na Mkoani Njombe Walalamika Kukosa Umeme Wa REA
Wananchi wa kijiji cha Ihanga’na kata ya Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe wameiomba serikali kupitia shirika la umeme Tanesco  kufikisha huduma ya umeme katika kitongoji A ambacho licha ya kupitiwa na miundombinu lakini hakijaunganishwa na huduma hiyo.

Kitongoji hicho chenye kaya zaidi ya 100 zenye uhitaji wa umeme kimedaiwa kushindwa kuendelea kiuchumi ikilinganishwa na maeneo mengine ya kata hiyo kwa sababu ya kukosa nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara.

Wakizungumzia changamoto hiyo wakazi hao wamesema wanashangazwa na kitendo cha miundombinu ya  umeme kupita katika  makazi yao lakini hawanufaiki nayo licha ya viongozi wa serikali akiwemo waziri wa nishati kuhimiza vijiji vinavyopitiwa kuunganishwa na nishati hiyo.

“Tunaumia sana na tunauhitaji na umeme sana hata mheshimiwa Rais kwenye vyombo vya habari  tulimuona umeme huu ni nyumba kwa nyumba hata kama nyumba iwe ya nyasi sasa tunashanga huu umeme umefika tunasikia unaishia huko juu na wanasema huu umeme utaishia kilomita kadhaa tu sisi tunajiuliza ni akina nani mpaka tukose,na sisi tunatamani tuonje huu umeme kwani sisi sio watanzania”walisema baadhi ya wananchi

Wakazi hao ambao wanategemea zaidi kilimo cha chai na parachichi wanadai wanashindwa kuongeza thamani ya mazao yao.

Mpekuzi blog imezungumza na Kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa Njombe mhandisi  Yusuph Salimu ambapo amesema kuwa serikali itasambaza umeme katika kaya zote za vijijini kupitia miradi ya REA  mzunguko wa tatu.

“Kwa sasa hivi kijiji cha Ihanang’ana B tayari wananchi watapata umeme mpaka kwenye mashule lakini Ihang’ana A kutokana na umbali tayari tumewaingiza kwenye Rea tatu mzunguko wa pili kwa hiyo ni mategemeo baada ya  mwaka wa bajeti kuanza maana yake utekelezaji wa maeneo hayo pia utafuata”alisema mhandisi Yusuph

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad