Baada ya kuenea na kuwepo kwa Maandamano ya vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo na Vyama vya upinzani kudai kutaka kuandamana leo jijini Dodoma kutaka kulishinikiza Bunge kufuta azimio lake la kutofanya kazi na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Prof. Musa Assad Jeshi la Polisi limeimarisha Ulinzi kila kona ya Mji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto, Akizungumza na waandishi wahabari leo amesema kuwa Makao makuu ya Nchi ni lazima yalindwe kwa gharama yeyote ambapo Jeshi leo limeimarisha ulinzi kila kona ya mji kutokana na tukio la Chama cha ACT-Wazalendo pamoja na Vyama vya Upinzani kutaka kuandamana.
Kutoka na hali hiyo Kamanda Muroto amesema kuwa Mkoa wa Dodoma ni Makao makuu ya nchi hivyo jeshi la Polisi halitakuwa tayari kumvumilia mtu yeyote atakayetaka kuvuruga amani kwa kisingizio chochote kile.
“Kama mnakumbuka jana wakati naongea nanyi ndugu waandishi wa habari kuwa watapigwa hadi wachakae tulikuwa hatutanii hivyo kama wangeweza kuingia barabarani kuandamana leo wangeona kipigo chao”amesisitiza Muroto.
Muroto amesema kuwa Jeshi la Polisi tangu leo asubuhi limeibarisha ulinzi kila kona ya mji kwa kutumia akari wa vikosi vya Mbwa na Farasi,Askari kanzu pamoja na kikosi cha FUU kwa kuzunguka maeneo ya mji .
“Nashukuru Mungu mpaka muda huu hakuna aliyeingia mtaani kuandamana ,nadhani wametii wangejaribu wangekumbana na kipigo na wangechakaa bila huruma kwa njia yoyote wasingepona ”amesema Muroto.
Ulinzi huo Uumeimarishwa kutokana na chama cha ACT- Wazalendo pamoja na Vyama vingine vya upinzani vya NCCR Mageuzi,Chauma na UPDP kutaka kuandamana kwenda Bungeni kushinikiza kufanyakazi na CAG Prof Musa Assad.