Waratibu wa maandamano Sudan kutangaza baraza la kiraia Jumapili

Waratibu wa maandamano nchini Sudan wamesema watatangaza baraza la mpito wanalotaka lichukue mamlaka kutoka kwa jeshi lililomuondoa madarakani rais Omar al-Bashir baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kumpinga.

Waratibu hao ambao wamekuwa nyuma ya maandamano hayo ya miezi minne wamechapisha taarifa yao hiyo leo inayosema watatangaza kuundwa kwa baraza hilo la kiraia watakapokutana na waandishi wa habari siku ya Jumapili.

 Jeshi la Sudan lilimuondoa rais Bashir wiki iliyopita na kuunda baraza la mpito la kijeshi kutawala nchini humo kwa kipindi kisichozidi miaka miwili lakini waandamanaji wamekuwa wakishinikiza kuundwa kwa baraza la mpito la kiraia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad