Wawili Watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya

Wawili Watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za biashara haramu ya dawa za kulevya
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limewakamata watu wawili kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo kwa hapa nchini ni kinyumke cha sheria.

Akitibitisha kukamatwa kwa madawa hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga alisema, huko katika Wilaya ya Kiteto alikamatwa Ramadhani Kombo (20) akiwa na kete 24 za bangi wakati anapekuliwa ili kuingizwa mahabusu kwa kosa la uvunjaji ikiwa ni kosa  lingine la aina hiyo kwa mtuhumiwa huyo.

Aidha, katika mji mdogo wa Mirerani katika geti la kuingilia kwenye machimbo ya Tanzanite wakati wa upekuzi wa kawaida walimkamata Jacob Ngoti (43) akiwa na misokoto 1,248 yenye uzito wa kilo 2.740 akiwa ameiweka kwenye begi la nguo la mgongoni ili asiweze kugundulika kirahisi.

Madawa hayo, alikuwa anakwenda kuwauzia wachimbaji wanaofanya kazi za uchimbaji ndani ya ukuta wa madini maarufu kama ukuta

Kamanda wa Polisi Augustino Senga alisema kuwa, jeshi hilo lipo makini na halitamvumilia mtu yeyote anayejishugulisha na uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad