Waziri Jafo Afunguka Kuhusu Kauli ya RPC Muroto 'Kuchakaza' Watakaoandamana

Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja, amehoiji serikali kuhusu kauli ya RPC kwamba wananchi wakiandama na watapigwa wachakazwe na kwamba kazi ya RPC ni ipi kwa wananchi wanaolipa kodi ili wao walipwe mishara?

Akijibu swali hilo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema kwamba wananchi kutii sheria bila shuruti ili kuweza kuepuka migongano isiyo ya lazima.

Jafo amesema, "jambo la kwanza kama taifa ni kushirikiana kila eneo. Vyombo vingine vinaongozwa kwa sheria, taratibu na kanuni na haswa katika suala la mambo ya ndani na sitaki kuingilia"

"Imani yangu ni kwamba wananchi watafuata taratibu, wa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migongano inayoonekana siyo ya lazima kwa afya ya taifa letu" amesema.

Siku ya jana Kamanda wa Polisi Gilles Muroto aliwaonya Vijana wa Jumuiya ya ACT - Wazaleondo na vyama vingine vya upinzani waliopanga kufanya maandamano leo Aprili 9, 2019 kusitisha maandamano yao, wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa.

Mbali na hilo Waziri Jafo amekiri kwamba wapo viongozi wa Mkoa na Wilaya ambao wanafanya vibaya na wapo kwenye tathmini.

"Hali ilikuwa mbaya, tulikuwa na MaDC na MaRC wanaofanya vibaya,sisi ndani tunafanya tathmini, tuvute subira" amesema Waziri Jafo.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad