Waziri Mkuu wa Ethiopia afanya Mazungumzo na Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan

Waziri Mkuu wa Ethiopia afanya mazungumzo na Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amefanya mazungumzo na ujumbe wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan ikiwa ni wiki moja tangu kupinduliwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar al Bashir.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Ahmed wa mtandao wa Facebook, ujumbe huo ulioongozwa na Jenerali Galaledin Alsheikh umelenga kumpa taarifa za hali inavyoendelea nchini Sudan ikizingatiwa umuhimu wa uhusiano muhimu baina ya nchi hizo.

Ujumbe huo umeitaka serikali ya Ethiopia kuendelea kuiunga mkono Sudan hususani katika kipindi hiki cha mpito.

Naye Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameuahidi ujumbe huo kuendelea kuiunga mkono Sudan na kusisitiza Baraza la Mpito la Kijeshi linaloongoza nchini Sudan linapaswa kuwa jumuishi katika kutatua na kusikiliza kilio cha wananchi wa Sudan.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad