Waziri Mkuu wa Mali Ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Mali ajiuzulu
Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu na baraza lake zima la mawaziri.

Soumeylou Boubeye Maiga alichukuwa hatua hiyo hapo jana, kufuatia wiki mbili za maandamano ya umma dhidi ya mauaji ya kiholela katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

 Maandamano hayo yalichochewa na mauaji ya wachungaji 160 wa jamii ya Fulani, ambayo yanashukiwa kufanywa na watu wa jamii ya Dogon, wanaoishi kwa kilimo na uwindaji.

Mauaji hayo yaliitikisa Mali, ambayo katika miezi ya karibuni imeshuhudia mauaji mengine kadhaa, yakiwemo yale ya wanajeshi 23 walioshambuliwa kwenye kituo chao.

 Juzi Jumatano, bunge lilijadili uwezakano wa kura ya kutokuwa na imani na serikali kutokana na mauaji hayo na pia kushindwa kuwanyang'anya silaha na kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali. Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 16,000 nchini Mali, vikiwemo vikosi kutoka Ufaransa na Ujerumani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad