Akizungumza jijini Hapa waziri Ummy amesema kuwa Bodi ina jukumu la kutoa miongozo ya kisera pamoja na kuchunguza na kuhoji ili kuhakikisha uzingatiaji wa katiba za mashirika yasiyo ya kiserikali.
Aidha, Waziri ummy ameongeza kuwa ni wajibu wa bodi hiyo kujielekeza katika kuhakikisha sekta hiyo inajiendesha kwa misingi ya uwazi na uwajibikaji ndani ya serikali , ndani ya mashirika yasiyo ya kiserikali na kwenye sekta binafsi.
Mbali na hilo waziri Ummy amesema bodi hiyo itafanya kazi kwa kuzingatia sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali lakini pia kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni zilizoko.
Rukia masasi ni mwenyekiti Bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali aliyemaliza muda wake amesema kuwa bodi ni chombo muhimu kwasababu inabeba NGO’s na ni mwakilishi wa asasi za kiraia ,NGO’s na pia ni mwakilishi wa serikali hivyo ni kama kiungo kwani serikali na asasi za kiraia,NGO’s ni wadau wanaoshirikiana katika maendeleo .
Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto anayeshughulikia idara kuu ya maendeleo ya jamii, Dkt John Jingu amesema sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali ni sekta ambayo inamchanganyiko wa kipekee kwani ni sekta kubwa na nipana.
Naye Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Richard Sambaiga amesema jukumu lao kubwa ni kuwezesha uratibu na utendaji kazi wa sekta hiyo ili uweze kustawi kwa maslahi ya umma wa Tanzania.
Hatahivyo, Waziri ummy amesema asasi za kiraia ,NGO’s ni sekta kubwa na nimuhimu katika kujenga na kushiriki katika Maendeleo ya kiuchumi,kisiasa ,kijamii na kiutamaduni.