Yanga Yafunguka Juu ya Matajiri wa Bilioni 200

Yanga Yafunguka Juu ya Matajiri wa Bilioni 200
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zenye kuleta mkanganyiko kwa mashabiki wa soka hasa wa klabu ya Yanga kuhusu klabu yao.

Taarifa hizo nyingi zinaenezwa katika mitandao ya kijamii, ambapo kurasa mbalimbali zinatoa taarifa za usajili kuelekea msimu ujao na michango ya klabu hiyo inayoendelea hivi sasa ambazo baadaye ziankuja kukanushwa na uongozi wa klabu.

Jana April 22 klabu ya Yanga imekanusha taarifa mbili zilizosambazwa na page ambazo si rasmi za klabu hiyo katika mitandao ya kijamii. Taarifa ya kwanza ni kuhusu usajili wa mchezaji Jacques Tuyisenge kutoka klabu ya Gor Mahia, ambapo ukurasa huo wa Facebook ambao sio rasmi uliweka picha yake na kuweka maneno "time will tell" yakimaanisha kuwa muda utazungumza.

Taarifa nyingine ya pili ambayo Yanga imeikanusha kupitia ukurasa wake wa Instagram ni ya michango, ambapo taarifa hiyo 'fake' imeeleza kuwa kamati ya michango imekamilisha mkakakati kwa asilimia 100 na kufikisha jumla ya Tsh. Bilioni 2 na kuongeza kuwa imeshapokea barua tatu kutoka kwa matajiri wanaotaka kuwekeza katika klabu hiyo huku kila mmoja akiwa na ofa ya Tsh Bilioni 200.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad