Zimbabwe Yatoa Tahadhari ya Athari za Kimbunga Kenneth...Kwa sasa Kimeshatua visiwani Comoro

Taarifa ya wizara ya habari Zimbabawe imeeleza kwamba Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa kutua Msumbiji Malawi na baadhi ya maeneo ya Zimbabawe, kimeshuhudiwa visiwani Comoros.

Imeeleza kwamba kutokana na uzoefu wa mkasa na athari ya kimbunga Idai mwezi uliopita, watu wote wanaoishi katika maeneo yalio katika hatari ya kukumbwa na mafuriko kama Mbire Muzarabani na maeneo ya chini ya jimbo la Masvingo na kwingineko, wanapaswa kujihadhari pakubwa.

Kimbunga hicho kimefika daraja la nne kikiambatana na upepo wa kasi ya 130 mph karibu na eneo la kati na kinaarifiwa kuelekea Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad