Alichokisema Maalim Seif baada ya Mdude wa Chadema kupatikana

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF ambaye kwa sasa amejiunga na ACT Wazalendo, Maalim Seif amesema kuwa ameamka na faraja baada ya kupatikana kwa Kada wa Chadema, Mdude Nyagali (Mdude Chadema) iliyedaiwa kutekwa.

Maalim Seif amesema kuwa ameumizwa na hali yake mbaya inayoashiria mateso aliyopitia.

"Nimeamka na faraja kufuatia taarifa za kupatikana Mdude Nyagali baada ya kampeni kubwa ya #BringBackMdudeAlive. Nimeumizwa na hali yake mbaya inayoashiria mateso aliyopitia," aliandika Maalim Seif kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Wito wangu kwa Watanzania sasa ni kuungana kudai uchunguzi huru wa kimataifa ufanyike kuhusu matukio haya."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad