Jamii ya wahindi wa tabaka la chini linalojukina kama Dalit linaomboleza kifo cha mmoja wao aliyeuawa kwa kosa la ''kukalia kiti na kula'' mbele ya watu wa tabaka la juu katika kijiji cha Kot nchini India.
Mwezi uliyopita kundi la wanaume wa jamii ya wahindi wa tabaka la juu lilidaiwa kumpiga vibaya mtu aliyefahamika kama Jitendra mwenye umri wa miaka 21 ili kumuadhibu lakini alifariki siku 9 baadae.
Hakuna hata mmoja kati ya mamia ya wageni waliohudhuria harusi hiyo aliyejitokeza kuelezea masaibu yaliyomkuta Jitendra siku ya April 26.
Chakula katika harusi hiyo kilipikwa na watu wa jamii ya tabaka la juu kwasababu watu katika kijiji hicho hawagusi chakula kilichopikwa na Dalit ambao zamani waliitwa "wasio guswa".
"Mzozo uliibuka wakati chakula kilipokua kikipakuliwa kuhusu nani aliyekalia kiti," afisa wa polisi Ashok Kumar alisema.
Geeta Devi anasema alimpata mwanawe akiwa amejeruhiwa nje ya nyumba yao
Ameongeza kuwa kisa hicho kimerekodiwa chini ya sheria (kupinga udhalimu) - iliyotungwa kuzilinda jamii zilizobaguliwa kihistoria nchini India.
Watu wa jamii ya Dalits, wamekuwa wakibaguliwa kwa muda mrefu nchini humo na jamii za matabaka ya juu.
Wakazi wa kijiji hicho kutoka jamii ya Dalit wanadai kuwa Jitendra alipigwa na kudhalilishwa harusini.
Ajikata kidole baada ya kukipigia kura chama asichokitaka
Taifa ambalo ni lazima kumuoa mwanamke uliyefanya naye ngono
Wanasema aliondoka katika sherehe hiyo akilia machozi, lakini aliviziwa na kushambuliawa tena hatua chache kutoka mahali hapo na kupigwa vibaya sana.
"Huenda alilala hapo usiku kucha," alisema huku akionesha mahali alipomkuta. "alikuwa na majeraha na alama kila mahali mwilini mwake. Nilijaribu kusema nae lakini hakuweza kunijibu."
Bi Geeta Devi, hajui ni nani aliyemuacha mwanawe nje ya nyumba yao. Alifariki dunia siku tisa baadae akipokea matibabu hospitali
Kifo cha Jitendra ni pigo kwa mama yake ambaye alimpoteza mume wake karibu miaka mitano iliyopita.
Kati ya familia 50 zinazoishi katika kijiji cha kina Jitendra, ni familia 12 ama 13 ndio wa tabaka la chini la Dalit.
Polisi imewakamata watu saba wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha Jitendra lakini wote wamekanusha kuhusika na kisa hicho.
"Hii ni hujuma dhidi ya familia yetu," alisema mmoja wa mwanamke ambaye baba yake, ndugu zake na wajomba zake wanatuhumiwa kutekeleza uovu huo.
"Kwanini baba yangu atumie suala l matabaka katika harusi ya Dalit ?" aliuliza mwanamke huyo.
Lakini jamii ya Dalit katika kijiji hicho ambao walishuhudia kifo cha Jitendra, wanapinga vikali madai hayo.
Auawa Baada ya Kukutwa kakalia Kiti na Kula Chakula Mbele ya Watu
0
May 21, 2019
Tags