Aunt Ezekiel Afunguka Kuhusu Mwanaye Cookie

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu. Kawaida ya safu hii ni kuwadadavua mastaa mbalimbali wa Bongo na kujua maisha yao halisi wanayoishi na watoto wao.

Leo ndani ya safu hii tunaye staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel, ambaye amejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Cookie. Mtoto huyu ni zao la dansa wa mwanamuziki Diamond, Moze Iyobo na Aunt.



Aunt amefunguka mengi ikiwemo jinsi anavyoishi maisha yake na mtoto wake huyo, fuatilia hapa chini…

Wikienda: Cookie kwako unamchukuliaje licha ya kwamba ni mwanao?

Aunt: Cookie kwanza ni rafiki yangu mkubwa sana, kingine ni mwalimu wangu.

Wikienda: Ukisema mwalimu wako unamaanisha nini?



Aunt: Unajua mtoto wangu kuna wakati anapenda wote tuzungumze lugha ya Kingereza kwa hiyo nikimwambia tuongee, anacheka kisha anaanza kunifundisha.

Wikienda: Mara nyingi unasafiri huku na kule, vipi kwa upande wa Cookie inakuwaje?

Aunt: Ninapoondoka lazima najua nimemuacha mtu ambaye anaeleweka na hata nikirudi mtoto wangu anakuwa salama tu.



Wikienda: Najua hivi sasa huishi na baba yake lakini toka huko nyuma alionekana wazi mtoto anampenda sana baba yake, hii hali inakuaje kwa sasa ambapo hampo pamoja?

Aunt: Kuna vitu ful-ani vinap-otokea huwezi kuvizuia ila baba yake anamuona kila siku kwa maana anampeleka shule na kumrudisha, ingawa atagundua kuna utofauti.



Wikienda: Kitu gani unachokiona kwa Cookie kila unapoishi naye na jinsi anavyokua?

Aunt: Kwanza kabisa ni mtoto anayenipenda sana na kingine atakuja kuwa mtu mwenye upendo wa hali ya juu na kila siku namuombea kwa Mungu akue katika hilo.

Wikiendi: Unawezaje kwa sasa kuwa peke yako bila baba yake?



Aunt: Yaani huelewi tu, Cookie ndio taa yangu anapokuwepo yeye kila kitu kipo sawa tu.

Wiki-enda: Una mpango wa kuzaa mtoto mwingine?

Aunt: Kwa sasa sijui, ila kiukweli sina ratiba hiyo kwenye kichwa changu.

Wikienda: Hakuna ugumu wowote kwenye malezi ukiwa mwenyewe?



Aunt: Hapana, mimi naona ni kawaida tu.

Wikienda: Watu wengi kwenye mtandao wanalaumu kumsuka mtoto nywele za watu wazima, unazungumziaje hilo?

Aunt: Unajua yule ni mtoto wangu, nina maamuzi yangu maana hao mama wa mitandao wamenichosha, waniache na mwanangu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad