Waziri Mstaafu wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Wenzake wamedhaminiwa na Wadhamini 2 huku yeye akidhaminiwa na Wadhamini 3, kila mmoja Tsh. Milioni 5.
Wanatakiwa kuripoti Kituo cha Polisi, Singida Mjini kesho saa 3
Akizungumzia tukio hilo, Nyalandu amesema alikamatwa jana saa 8 mchana akiwa kwenye kikao cha ndani na vijana 29 katika kijiji cha Itaja jimbo la Singida Kaskazini.
Amesema walivamiwa na watu walioanza kuuliza alipo Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaban Lyimo ambaye alisimama na kuwaeleza watu hao kuwa walikuwa katika kikao cha ndani cha Chadema.
“Kwanza walituliza kibali (cha kikao), Lyimo akawajibu kuwa hatuna na ni kikao cha ndani hakihitaji kibali. Wakasema kuwa wao wametoka Takukuru Mkoa wanawahitaji watu wakaninyooshea kidole mimi (Nyalandu) na David Jumbe pamoja na mwenyekiti (Lyimo),” amesema Nyalandu.
Amesema walielezwa kuwa wanahitajika kwa ajili ya mahojiano Singida mjini na walipofika wakaelezwa kuwa wanafuatilia masuala ya rushwa.
“Tulipofika polisi tulihojiwa zaidi ya masaa mawili tukapewa dhamana ilikuwa imefika saa 4 usiku tuliambiwa kwamba twende kisha turudi asubuhi (leo), wakati tukijiandaa kuondoka, mkuu wa kile kituo akapigiwa simu na kutakiwa kufuta dhamana zetu, hivyo tukalala ndani hadi leo.”
Baada ya Kaachiwa kwa Dhamana Nyarandu Asimulia Yaliyomkuta
0
May 29, 2019
Tags