Barcelona Yaitandika Liverpool Mabao 3-0

MABAO mawili ya Lionel Messi yaliisaidia Barcelona kusafi sha njia ya kutinga fainali baada ya kuicharaza Liverpool mabao 3-0 kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa jana katika uwanja wa Nou Camp.



Kwa matokeo hayo sasa, Barcelona inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote ugenini wakati timu hizo zitakaporudiana Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Anfield.


Liverpool kwa kipigo hicho wamejiweka pabaya kwani wanatakiwa kushinda kuanzia mabao 4-0 na kuendelea ili kutinga fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Juni 1, mwaka huu kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid.



Mshindi wa baina ya timu hizo atavaana na kinara wa mechi nyingine nusu fainali kati ya Ajax Amsterdam iliyoichapa Tottenham Hotspur ugenini bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa White Hart Lane jijini London.


Messi aliudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni mwanasoka bora duniani baada ya kupachika mabao mawili wakati jingine likipachikwa na Luis Suarez.

Barcelona, ambayo ilikuwa ikicheza kwa kuchanganya soka ya pasi na mashambulizi ya kushitukiza `counter attack’, ilipata bao la kuongoza mnamo dakika ya 26 likipachikwa na Suarez ambaye aliunganisha mpira wavuni kutokana na krosi maridadi ya Jordi Alba na mpira kumshinda kipa wa Liverpool, Alisson.


Messi alipachika bao la pili la Barcelona mnamo dakika ya 75 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba kufuatia shuti la Suarez. Bao la tatu la Barcelona lilikuwa kali zaidi kwani Messi alipachika bao lake kwa `freekick’ ambapo mpira ulipita kwenye `nyuzi 90’ ya mwamba wa goli kipa wa Liverpool, Alisson alichupa bila ya mafanikio ya kuokoa. Pamoja na matokeo hayo, mchezo kwa ujumla ulikuwa mkali huku timu zote zikishambuliana vikali kwa pasi na mashambulizi ya `counter attack.’


Timu hizo zilianza kwa kasi mchezo huo, ambapo Barcelona ingeweza kupata bao mapema dakika ya tatu baada ya pasi ya kiungo wake, Ivan Rakitic kukosa mtu wa kuunganisha kwenye eneo la Liverpool, ambapo mpira uliokolewa na beki Joel Matip na kuwa kona.



Liverpool, ambayo kwa mara ya kwanza imepoteza mchezo kwenye Uwanja wa Nou Camp, ililalamikia kunyimwa penalti na mwamuzi mholanzi Bjorn Kuipers katika dakika ya tano baada ya kudai straika wao Sadio Mane aliangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Barcelona, Gerard Pique. Pia straika wa Liverpool, Mohamed Salah alifanya kazi nzuri ya kukimbia na mpira kutoka katikati ya uwanja lakini pasi yake iliokolewa na mabeki wa Barcelona kwenye eneo lao katika dakika ya 11.



Barcelona nayo ilijibu mapigo kwa kufanya shambulizi katika dakika ya 14 lakini beki wa Liverpool, Andy Robertson aliokoa hatari kutoka kwa Messi, ambaye hata hivyo alidai beki Matip alinawa mpira kwenye eneo la penalti wakati wakikabiliana.


Mane alikosa nafasi nzuri ya kusawazishia timu yake baada ya kupaisha mpira akiwa na kipa Marc-Andre Ter Stegen katika dakika ya 35 baada ya kuwahi mpira aliokuwa ametanguliziwa.



Liverpool ilipoteza nafasi nyingine nzuri angalau ya kupata bao la kufuatia machozi mnamo dakika ya 85 baada ya shuti la Salah kugonga mwamba baada ya kupata mpira uliookolewa na mabeki wa Barcelona kufuatia shuti la straika mwenzake, Roberto Firmino.

Barcelona:

Ter Stegen (8), Roberto (6.5) (Alena), Piqué (7.5), Lenglet (6), Alba (8), Rakitic (7), Busquets (5.5), Vidal (7), Messi (9), Suárez (8.5) (Dembele), Coutinho (5) (Semedo)

Unused substitutes:

Arthur, Cillessen, Malcom, Umtiti,

Bookings: Lenglet, Alba, Suarez

Goals: Suarez (26), Messi (75, 82)

Liverpool:

Alisson (6.5), Gomez (6.5), Matip (6.5), Van Dijk (7.5), Robertson (7), Milner (7) (Origi), Fabinho (7.5), Wijnaldum (6)(Firmino), Salah (7), Mané (8), Keita (6) (Henderson)

Unused substitutes:

Lovren, Mignolet, Shaqiri, Alexander-Arnold

Bookings: Fabinho

Referee: Bjorn Kjupers

Attendance: 98,289
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad