Birthday ya Ruge: Mwachi aeleza ukaribu wa Nandy na Ruge ‘Nandy alimpenda sana baba


Leo Mei Mosi ambayo ni siku ya wafanyakazi ni siku ya kuzaliwa ya marehemu Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media. Alifariki dunia Februari, 26 akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini na baada ya siku chache kuzikwa nyumbani kwao Bukoba.



Leo ni siku yake ya kuzaliwa ambapo wadau mbalimbali wakitoa salamu zao ambapo shughuli ya ibada itafanyika nyumbani kwao Bukoba.

Katika maandalizi ya shughuli hiyo, Mwachi ambaye ni mtoto wa marehemu amefunguka kwa mara ya kwanza kumzungumzia muimbaji Nandy ambaye ameonekana kuwa karibu zaidi na familia hiyo.

“Nandy alikuwa ana uhusiano na baba yangu,” alisema Mwachi wakati akizungumza na Millardayo TV. “Nimeanza kumjua kupitia hilo ingawa alikuwa msanii wa THT, kwahiyo kwa familia tumemfamu kama mpenzi wa baba wangu na alikuwa ana muheshimu sana baba yangu na sisi tumeamua kumheshimu,”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad