Bobi Wine Aachiwa Huru kwa Dhamana Uganda Apewa Masharti Magumu

Msanii na mwanasiasa wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi ameachiwa kwa dhamana na mahakama mjini Kampala japo kwa masharti makali.

Mchakato wa kulisikiliza ombi lake la dhamana uliendeshwa kwa njia ya video akiwa gerezani Luzira.

Aliweza kuwasiliana na hakimu kupitia mawasiliano hayo ya video, hatua ilioepusha kutokea kwa vurugu kama ilivyotarajiwa iwapo angasafirishwa hadi mahakamani.

Ameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya 'haramu' mnamo mwaka jana ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT.


Wafuasi wa mbunge Robert Kyagulanyi walionekana wakiimba wimbo wao wa ushindi baada ya hakimu wa mahakama ya Buganda Road kukubali ombi la Bobi Wine kupewa dhamana.

Kesi iliendeshwa kwa njia ya video wakati Bobi Wine akiwa gerezani Luzira
Uamuzi huo ulitolewa katika kikao kilichochukua muda wa saa nne, upande wa serikali ukipinga apewe dhamana.

Kabla ya hakimu kumpatia dhamana, Bobi Wine alipewa fursu ya kuzungumuza:

'Napenda kusisitiza kwamba sio mimi ninayeshitakiwa mahakamani ni mahakama yenyewe, maamuzi ya mahakama itakayotowa sio tatizo kwangu, mimi nitaendelea na kusema ukweli.

'Kazi yangu ni kutetea haki, kazi yangu ni kupigania haki yako wewe hakimu na mimi na raia wengine wa Uganda. Kama itakuwa haki mimi kubaki hapa korokoroni, nitamushukuru mwenyezi Mungu kwa sababu nina kazi nyingi za kufanya hata hapa gerezani' alisema mwansiasa huyo wa upinzani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad