Bunge Latoa Rambirambi Kufuatia Kifo Cha Reginald Mengi

Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa niaba ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameungana na Watanzania kuomboleza kifo cha Dkt. Reginald Mengi na kueleza mchango wake mkubwa kwa taifa.

Spika Ndugai ametumia dakika mbili kuoeleza mchango wa Dkt. Mengi katika Taifa na namna wakavyomkumbuka.

"Katika kuomboleza kifo sisi Bunge tunaungana na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, familia ya marehemu na Watanzania wote tukimshukuru Mwenyenzi Mungu na kumshukuru Mhe. Mengi kwa mchango wake mkubwa usiopimika kwetu Watanzania," amesema Spika.

Dkt. Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, alifariki usiku wa kuamkia jana akiwa Dubai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad