Serikali Yawataka Wananchi Waoishi Karibu Na Migodi Mikubwa Ya Dhahabu Kuacha Utegemezi.

Serikali Yawataka Wananchi Waoishi Karibu Na Migodi Mikubwa Ya Dhahabu Kuacha Utegemezi.
Serikali  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  imewataka wananchi wanaoishi karibu na Migodi mikubwa ya Madini ya (Buzwagi na Bulyankulu ) kufanya kazi zingine mbadala za kuwaingizia vipato badala ya kutegemea ajira katika  migodi hiyo ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na tija baina yao na wawekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na jana na Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA katika Hafla maalum ya kumtambulisha Mzabuni aliyeshinda Dhabuni ya kuzoa Taka ngumu hususani  vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu, AZAN LOGISTIC CO.LTD ya Kahama.

Amesema kuwa baada ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wa madini katika migodi hiyo baadhi ya wananchi wanao ishi karibu Migodi hiyo wamekuwa tegemezi kwa kutojihusisha na kazi zingine  za uzalishaji mali na kuwataka wafanye kazi za ujasiriamali.

Katika Hatua nyingine MACHA ameitaka Kampuni ya AZAN LOGISTIC  kutoa ajira kwa Wazawa pindi atakapoa anza kutoa huduma hiyo katika mgodi huo ili kuwapa hamasa wananchi kupenda kufanya kazi na  wawekezaji wazawa.

 Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo,  AZAN SAID SALUM ameahidi  kutoa ushirikiano kwa wananchi wa Mji mdogo wa  Kakola ambapo Mgodi huo upo  na kuahidi kuwa kampuni yake itaajiri walimu wawili wa sayansi katika shule mbili za sekondari katika Halmashauri ya Mslala.

Mbali na hilo  Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Msalala, SAIMON BEREGE  ametolea ufafanuzi suala la upimaji wa viwanja kwa kusema kuwa tayari Kampuni za upimaji zinaendelea na upimaji  ili kuhakikisha wananchi wanarasimishiwa makazi yao ambapo kwa awali viwanja elfu 10 vitapimwa.

Kampuni ya AZAN LOGISTICS imeshida  dhabuni hiyo ambapo kwa sasa itatoa huduma ya kuzoa vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu kwa Muda wa Mwaka mmoja na miezi 10.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad