Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya England, David Beckham amepigwa marufuku kuendesha gari kwa miezi 6 baada ya kupatikana na kosa la kutumia simu wakati akiendesha gari.
Mbali na adhabu hiyo, Mahakama mjini London imempiga faini ya £750, na kuagizwa alipe £100 gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 katika siku saba zijazo.
Jaji katika mahakama hiyo amemuambia hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni ‘hakuna kisingizio’ chini ya sheria.
Mwendesha mashtaka amesema: “Badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama simu mapajani mwake.”
Nchini Uingereza kushika simu ukiwa unaendesha gari ni kosa unaweza kuadhibiwa kwa kupunguziwa pointi kwenye leseni na kutozwa faini ya £20
Wakili wa Beckham Gerrard Tyrrell amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ” haikumbuki siku hiyo au tukio hilo”.
Mahakama imeeleza picha hiyo alipigwa na raia akiwa ameshikilia simu wakati akiendesha gari lake aina ya Bentley ‘taratibu’ katika foleni.