Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten, ameweka wazi kuwa yeye haamini kama mashabiki wanaweza kwenda uwanjani kwa kuhamasisha na msemaji bali ni mapenzi yao kwa klabu ndiyo yanawapeleka uwanjani.
''Ninavyoamini mimi, mashabiki wa soka kwenda uwanjani ndiyo utamaduni halisi wa soka, ndiyo maana vilijengwa viwanja vya soka na si soka kuchezwa kwenye vituo vya daladala'', amesema.
Dismas ameeleza sababu nyingine ni kuwa na kikosi kizuri, imara chenye uhakika wa ushindi, wachezaji wazuri ambao ni brand, urahisi wa tiketi na usalama.
Ameongeza kuwa, ''Kitu muhimu ni klabu au timu kutengeneza mazingira mazuri ya kumfanya mtu kwenda uwanjani, huwezi kusema kwamba ili watu waende uwanjani ni lazima kuunda kamati''.
Kwa upande wake msemaji wa Simba Haji S Manara, huwa anaamini anafanya kazi kubwa ya kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani lakini Dismas anasema yeye siyo mmoja wa wanaoamini kuwa makelele ya mtu au mtu kukashifu wengine ndio sababu ya watu kwenda uwanjani. ''Haiwezi kuwa hivyo, siku mtu huyo asipokuwepo duniani viwanja vifungwe?.