Dk. Shein Akemea Suala la Wasanii Kuibiwa Kazi zao


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa ni jambo baya sana na halikubaliki katika jamii kwa wasanii kuibiwa kazi zao na wajanja wachache ambao hujinufaisha wao.

Dk. Shein aliyasema hayo katika ukumbi wa Ikulu ndogo Kibweni mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019.

Rais Dk. Shein alisema kuwa ni vyema sheria ikatazamwa na kama kuna haja ya kuangaliwa kwa kufanywa marekebisho basi ni vyema jambo hilo likafanyika kazi ipasavyo ili kuondosha kabisa dhulma hiyo wanayofanyiwa wasanii wakiwemow asanii wakongwe.

Alisema kuwa imekuwa ni utamaduni hivi sasa kwa baadhi ya watu kuzitumia kazi za wasanii kwa kujinufaisha wao huku wakiwaacha wasanii husika kutopata kipato ama faida zozote za kazi zao na badala yake wajanja hao wakajinufaisha wao.

Hivyo, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwekwa mikakati maalum katika kutafuta taratibu na ufumbuzi wa suala hilo kisheria na kusisitiza haja ya kutizamwa sheria iliopo hivi sasa kama inakidhi haja juu ya suala hilo ama inahitaji marekebisho.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza haja kwa uongozi wa Wizara hiyo kwa kupitia Idara yake ya Utamaduni na Sanaa ikalifanyia kazi suala zima la kivazi cha Mzanzibari mwanamke na mwanamme na jinsi kinavyovaliwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad