Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es salaam, Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.
Walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Islam aliyepata 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba kura 1,174, Dominick Ikute kura 1,088, Kamugisha Kalokola kura 1,072, Arafat Haji kura 1,024, Salum Ruvila kura 976, Saad Khimji kura 788 na Rodgers Gumbo kura 776.
Uchaguzi huu umefanyika kufutia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.
Pamoja na kuwa kocha wa Taifa Stars, Dk. Msolla pia amewahi kuwa mtumishi wa Serikali kwa nafasi mbalimbali, ikiwemo Ukurugenzi wa Uendelezaji wa Mazao katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakati wa awamu ya Nne chini ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.