Haji Manara Awaka "Shutuma Dhidi Yetu Zinatolewa Kihuni"

Shutuma zinazowakabili mabingwa watetezi wa   ligi kuu soka Tanzania Bara juu ya kutoa pesa ili kufanikiwa kushinda kwa timu zinazokutananazo zamuibua msemaji wao Haji Manara na kuahidi kuzungumzia.



Mara kadhaa Simba imekuwa ikishutumiwa kutumia fedha katika kununua baadhi ya mechi ili kufanikiwa kupata matoke jambo ambalo bado halina uhakika kwakuwa hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kujitekoza kuthibitisha hilo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara amesema kuwa kamwe hawezi kuzikalia kimya shutuma zinazoelekezwa dhidi yao.

”Kesho (leo) ntaongea na Press hapa Mbeya kuhusu mwenendo wa Ligi kuu na shutuma dhidi yetu zinatolewa kihuni huni!!,” amesema Manara

”Nnabutua bakuli. Sina uvumilivu huo ,wanaofikiri Simba ni dhaifu na unaweza kuitolea maneno ya kipumbav,kesho wasikilize moto, Klabu hii ina Msemaji very strong na mwenye kila neno liwe la kistaarabi hadi la kihuni!!,” ameandika Haji Manara kwenye akaunti yake ya Instagram.

View this post on Instagram

Wanahabari mliopo Mbeya saa nne kamili asubuhi ya leo ntazungumza nanyi hapo Sokoine Stadium Mbeya,ambapo kwa sasa Naibu Spika wetu Mh Tulia anamalizia mbio zake za Marathon!! Tukutane tuzungumzie ligi yetu kwa ujumla

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on May 3, 2019 at 11:08pm PDT

Msemaji huyo machachari wa wekundu wa Msimbazi Simba SC ameongeza ”Wanahabari mliopo mbeya,ofisi yetu itawafahamisha wapi na muda gani ntaongea,ila ntatema cheche,siku nyingi nimekaa kimya.”



Hapo jana baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo Sport BC vilimnukuu kocha mkuu wa klabu ya Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo akisema kuwa wamecheza mpira mzuri ila wayoshinda ni wenye pesa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad