Haji Manara wa Simba Aibua Gumzo Bungeni, Wizara Yatakiwa Kujifunza Kutoka Kwake


Dodoma. Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kujifunza kwa msemaji wa timu ya Simba, Haji Manara, kuhusu uhamasishaji anaoufanya kwa timu yake.

Chumi amemtaja Manara leo bungeni Alhamisi Mei 23, 2019 alipochangia hotuba ya wizara hiyo bungeni.

Amesema kama wizara hiyo itachukua mbinu ya mhamasishaji huyo inaweza kuwa imefanya vizuri na kujaza watalii nchini.

"Manara alihamasisha wakati Simba ikicheza na Uganda na tukajaza Uwanja wa Taifa, huyu ni mbunifu wa uhamasishaji katika kila eneo hivyo wizara ikiwa sawa na huyo inaweza kujaza watalii wengi," amesema Chumi.

Mbali na Manara lakini amewataja Thobias Kifaru wa timu ya Mtibwa na Masau Bwire ambaye ni msemaji wa timu ya Ruvu Shooting.

Kauli ya Chumi kuhusu Simba iliibua kelele za shangwe bungeni baada ya mwenyekiti wa bunge Mussa Zungu kutaka arudie kuitaja timu hiyo.

By Habel Chidawali,Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad