Hatimaye Mwinyi Zahera Afunguka Kuhusu ishu ya Makambo Kusajiliwa Horoya AC na Tetesi za Kuwa Wakala Wake

Hatimaye Mwinyi Zahera afunguka kuhusu ishu ya Makambo kusajiliwa Horoya AC.

Kwanza ni kweli wewe ni Wakala wa Makambo?

Mimi sio wakala wake. Ni yeye aliniomba nimsindikize baada ya kuona watu wengi wanamsumbua, sasa kwa kua nina uzoefu nikaona hakuna shida kwa sababu hakukua na mchezo wowote wa Yanga hapa karibuni.

Ni kweli Makambo yuko kwa Mkopo Yanga?

Sio kweli. Makambo kama atauzwa hela yote itaingia Yanga. Alitoka Congo akiwa mchezaji huru kabisa.

Vipi ameshamalizana na Horoya?

Sio kweli. Kule tulikwenda kuwasikiliza tu. Tumeongea nao na watakuja kumalizana na Yanga kama wanamuhitaji kweli. Unajua Makambo sio streka peke yake duniani hivyo tunaweza kumuuza na kununua mwingine.

Mbona kuna picha zimemuonyesha akisaini mkataba wa viongozi wa Horoya?

Sasa hilo swali kawaulize Horoya wenyewe. Waandishi ni waongo sana. Walishawahi kusema mimi nimeondoka Ulaya sitarudi tena Yanga. Mimi nakwambia Makambo ni mchezaji halali wa Yanga hayo mengine siyajui

Sehemu ya mahojiano ya Zahera na kituo cha WAPO REDIO.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad