Huawei Yasema Mabilioni ya Wateja Kuathirika na Hatua ya Marekani

Huawei yasema Mabilioni ya wateja kuathirika na hatua ya Marekani
Mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya China ya Huawei, amesema uamuzi wa Marekani kuiorodhesha katika makampuni yanayolengwa kibiashara itaathiri mabilioni ya watumiaji wake.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Song Liuping amesema katazo la kibiashara la Marekani pia litawaathiri moja kwa moja makampuni ya Kimarekani pamoja na ajira.

Huawei sasa inasema uamuzi wa Marekani kuiorodhesha kampuni yao kama moja ya makampuni mabaya kiusalama, inamadhara makubwa kuliko utawala wa Washington unavyokadiria.

"Uamuzi huu unatishia kuwadhuru zaidi ya wateja wetu katika nchi 170 duniani, wakiwemo watu bilioni tatu ambao wanatumia bidhaa na huduma za Huawei," imesema taarifa ya kampuni hiyo.

Hivi karibuni utawala wa Washington uliiorodhesha Huawei katika msururu wa makampuni ambayo Marekani imeyapiga marufuku kufanya nao biashara labda tu wapate leseni maalumu. Marekani ilichukua uamuzi wa kuizuia Huawei ambayo ni wazalishaji wakubwa duniani wa vifaa vya mawasiliano kwa kile ilichodai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikidukua taarifa na ni hatari kwa usalama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad