Watuhumiwa hao, Kevin Gonot, Leonard Lopez na Salim Machou wamepewa siku 30 za kukata rufaa huku Mahakama ikisema kuwa imeshawahukumu zaidi ya wageni 500 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa IS tangu mwaka 2018.
Raia hao watatu waliohukumiwa jana ni miongoni mwa Wafaransa 13 waliokamatwa katika mapambano huko Mashariki mwa Syria na kukabidhiwa kwa mamlaka za Iraq mwezi Februari, 2019.
Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International, Iraq ndio nchi inayoongoza katika utekelezaji wa adhabu ya kifo duniani na ilitangaza kuanza kuliangamiza kundi la IS mwishoni mwa mwaka 2017.