Iran yajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia,

Iran inasema itaongeza urutubishaji wa madini ya uranium baada ya siku 60, mwaka mmoja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo wa kimataifa.



Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Rais Hassan Rouhani amesema baada ya siku 60 Tehran itaongeza zaidi urutubishaji wa madini ya uranium yanayotengeneza nyuklia ambayo yamezuiwa na mkataba huo.

Mkataba huo unalenga kukabiliana na utengenezaji wa nyuklia ili iweze kuondolewa vikwazo vya misaada , lakini uhasama umeongezeka tangu Marekani ijiondoe

Uchumi wa Iran umeyumbishwa na vikwazo vipya vya Marekani dhidi yake.

Ni kwanini mpango wa nuklia umeingia kwenye mzozo?

Mkataba wa nyuklia uliokubaliwa na Iran na mataifa mengine matano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa -Marekani , Uingereza , Ufaransa , Uchina na Urusi – pamoja na Ujerumani – uliingia dosari pale rais wa Marekani Trump alipotangaza kujiondoa mwaka mmoja uliopita

Tangu wakati huo thamani ya fedha ya Iran iliporomoka kwa kiwango ambacho hakikuwahi kushuhudiwa, viwango vya mfumuko wa kiuchumi vya mwaka vilikuwa vikubwa na wawekezaji wa kigeni wakaihama nchi.

Nchi zinazounga mkono mkataba huo kutoka Ulaya, ambazo zilipinga vikwazo vipya dhidi ya Iran zimekuwa zikijaribu kutafuta njia za kuuendeleza.

Hii ni pamoja na kuanzisha mfumo maalumu wa malipo ya kusaidia makampuni ya kimataifa yanayotaka kuendelea kufanya biashara na Iran kwa kukiuka vikwazo.

Lakini pia nchi hizo ziliionya Iran kwamba inapaswa kuendelea kuheshimu vipengele vyote vya mkataba, hususan kipengele kinachohusiana na shughuli za nuklia.

Hata hivyo, chini ya mkataba unaofahamika kama Mpango wa pamoja wa utekelezaji (JCPOA) – Iran ilisema kuwa itachukulia kuanzishwa upya kwa vikwazo “kama sababu ya kuacha utekelezaji wa mkataba … wote au sehemu yake ”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad