Irene Uwoya Atoa Onyo Kali kwa Wanaomsema Vibaya Mwanaye


Msanii kutoka Bongo Movie, Irene Uwoya amewaonya wanaomsema vibaya mwanaye wa kiume, Krish kutokana na uzuri wake akiwaambia kuwa wakiendelea watakiona cha mtema kuni.

Irene amesema anaumizwa mno na watu wanaomsema vibaya Krish kwa maneno yasiyofaa kwa mtoto kwa sababu tu anaonekana mzuri hivyo kuahidi kuwaadabisha wanaofanya hivyo.

“Unakuta mtu anamuombea maneno mabaya Krish, eti kisa nimezaa mtoto mzuri, naomba waache na mtu akitaka kunivuruga, basi amuongelee Krish vibaya,” ameeleza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad