Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim amesema madereva wa serikali wanapaswa kufauata sheria kama watumiaji wengine wa barabarba.
Ameeleza hayo kupitia kipindi cha Hoja kwa Hoja cha Kwanza TV ambapo amesisitiza kuwa hata wanachukua hatua za kisheria huwa hakuna kosa dogo kwani likiachwa linaweza kuleta madhara makubwa.
"Madereva wa Serikali wanapaswa kufuata sheria za barabarani kama madereva wengie wanavyofuata sheria" amesema Kamanda Muslim.
"Hakuna kosa dogo katika masuala ya kisheria, hilo kosa dogo ambalo watu wanaliona linaweza kusababisha madhara makubwa sana" amesisitiza.
Pia Kamanda Muslim amesema ili kuhakikisha vitendo vya kutanua barabarani havitokei polisi wanachukua hatua kali sana.
"Rushwa ni makubaliano kati ya watu wawili, mtoaji na mpokeaji, kwahiyo kama dereva akatoa rushwa na askari akapokea rushwa wote ni wakosaji na wanavunja sheria" amesema.
Ameendelea kwa kusema,
"Huwezi kumuweka mtu mahabusu bila kosa, tunaangalia sheria inasemaje, huko nyuma sheria zilikuwa hazisimamiwi sasa baada ya kuanza kusimamia sheria watu ambao walikuwa hawakamatwi wakikamatwa ndio wanakuwa walalmikaji wakubwa,".