Jeshi la Polisi Lamuua Jambazi Sugu Mara

Jambazi sugu, Bahati Nyakiha 35 mkazi wa kijiji cha Nyarero kata ya Binagi wilayani Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo ameuawa kwenye majibizano makali na Jeshi la polisi huku akiwa na Bunduki na magazine moja yenye risasi zaidi ya 12.

Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ,Henry Mwaibambe amesema Jambazi huyo ameuawa na Askari polisi waliokuwa wakifuatilia nyendo za wahalifu waliokuwa wanataka kufanya uporaji katika duka moja kubwa la vifaa vya ujenzi.

“Leo majira ya saa saba usiku katika eneo la kijiji cha Nkerege Polisi wakiwa wanafuatilia nyendo za wahalifu waliokuwa wanataka kufanya uporaji katika moja wapo la Duka kubwa la vifaa vya ujenzi na baada ya watuhumiwa hao kuwaona Askari polisi wanawafuatilia walianza kujihami kwa kuwafyatulia risasi askari huku wakiwa wanakimbia ambapo polisi  walijibu mapigo na kufanikiwa kumpiga risasi maeneo ya mgongoni jambazi huyo na kuanguka chini”alisema Mwaibambe.

Mwaibambe aliongeza kuwa majambazi hao wakiwa katika mapambano ya majibizano makali  na Askrai polisi waliwafyatua Askari polisi risasi zaidi ya nane ambapo Askari walifanikiwa kumuua jambazi moja kwa kujihami.

Mwaibambe alifafanua kuwa inasadikiwa majambazi hao walikuwa takribani wanne ambapo askari polisi walifanikiwa kumpiga risasi mmoja wao huku wengine watatu wakifanikiwa kutorokea  kusiko julikana na Jeshi la polisi linaendelea kuwasaka ili kuwatia hatiani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad