Jeshi la Sudan lakataa kukabidhi utawala kwa raia

Afisa wa ngazi ya juu wa baraza la jeshi nchini Sudan ameiambia BBC kuwa haitaruhusu raia kuchukua nafasi za juu katika baraza la uongozi nchini humo wakati wa serikali la mpito.

Luteni generali Salah Abdelkhalek amesema kwamba labda wanaweza kuzingatia kuwapa nafasi sawa za ujumbe katika baraza hilo.

Waandamanaji wanaendelea kuandamana kwa kukaa kwa wingi nje ya ofisi kuu ya jeshi la nchini hiyo wakitaka kuachia madaraka.

Raisi Omar al-Bashir aliondolewa kwenye madaraka mwezi Aprili tarehe 11 baada ya kutawala Sudan kwa miaka 30.

Na Omar al Bashir aliondolewa madarakani na baraza la mpito la jeshi ambalo limechukua utawala kwa raia kwa kipindi cha miaka miwili, jambo ambalo linapingwa na waandamanaji

Waandamaji Sudan ''kutangaza serikali ya mpito'' Jumapili
Viongozi wa waandamanaji wamelishutumu jeshi kukataa kufanya majadiliano kwa nia njema na kuhamasisha maslahi ya Bashir.

Viongozi wa Jeshi wanasema kuwa wanahitajika kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kuwa wanaongoza na usalama wa taifa hilo.

Je kuna 'mkono' wa kigeni nchini Sudan?
Waandamanaji wakata ushirikiano na jeshi Sudan
Wajumbe saba wa baraza ambalo linaongozwa na Luteni generali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, ambaye aliiambia BBC mwezi uliopita kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kama watafikia makubaliano na viongozi wa uraia.

Viongozi wa upinzani walisema jana kuwa mapendekezo ya nakala ya katiba kwa baraza la jeshi kueleza mapendekezo waliokuwa nayo katika kipindi hiki cha uongozi wa mpito.

Wanasema kwa sasa wanasubiri majibu. Nakala ya mapendekezo na majukumu ya baraza jipya haijaainisha nani atakuepo katika baraza.

Umoja wa Afrika ilikabidhi utawala kwa viongozi wa jeshi tarehe 15 Aprili na sasa wana siku 60 au kukutana na baraza la uongozi.

Makao makuu ya jeshi la Sudan yana muonekano gani?

Picha iliyopigwa na satelite ikionyesha makao makuu ya jeshi katika makao makuu ya Khartoum, eneo ambalo waandamanaji walikusanyika na kubaini kuwa limetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuanza kazi ya utawala .

Kutoka angani , inaonyesha wazi picha inaonyesha wazi namna majengo ya jeshi yalivyofanana na muundo wa boti na kuonekana kama ndege.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad