Viongozi wa kijeshi wa Sudan wametangaza makubaliani na muungano wa upinzani juu ya kipindi cha mpito cha miaka mitatu kwa ajili ya kuukabidhi utawala wa kiraia.
baraza la kijeshi la mpito (TMC) limesema kuwa muungano utakuwa na theruthi mbili ya viti katika baraza la bunge.
Sudanimekuwa ikitawaliwa na baraza la jeshi ltangu mwezi uliopita baada ya mapinduzi ya rais Omar al-Bashir.
Maandamano yaliyosababisha kuanguka kwa utawala wake yamekuwa yakiendelea huku waandamanaji wakidai kuwekwa kwa serikali kamili ya kiraia.
Saa kadhaa kabla ya mkataba wa sasa kutangazwa, takriban waandamamnaji watano na afisa mmoja wa usalama walikufa katika makabilianokatika mji mkuu Khartoum.
Sita wauwawa katika maandamano Sudan
Wasifu wa Omar al-Bashir Sudan
Waandamanaji wakata ushirikiano na jeshi Sudan
Nini hasa walichokubaliana?
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Luteni Jenerali Yasser al-Atta alisema kuwa makubaliano ya mwisho juu ya mgawanyo wa madaraka yatasainiwa pamoja na upinzani - Azimio la the Declaration of Freedom na Change Forces (DFCF) - katika kipindi cha saa 24. makubaliano hayo yatajumuisha kubuniwa kwa baraza la kujitawala ambalo litaongoza taifa mpaka uchaguzi utakapofanyika.
"Tunaapa kwa watu wetu kwamba makubaliano yatakuwa yamekamilika katika kipindi cha saa 24 kwa njia inayotarajiwa na watu," alisema.
Jenerali Atta amesema kuwa DFCF utakuwa na theruthi mbili ya viti 300 vya bunge la mpito huku viti vilivyosalia vikichukuliwa na vyama ambavyo si sehemu ya muungano wa upinzani
Awali, msemaji wa vuguvugu la waandamanaji Taha Osman alisema kuwa pande zote zimekubaliana juu ya muundo wa mamlaka zijazo za utawala - baraza la utawala , bunge na baraza la mawaziri
Mjumbe wa DFCF Satea al-Hajj alielezea matumaini yake kuwa yaliyomo kwenye mkataba wa mwisho juu ya mgawanyo wa madaraka yatakubaliwa : "Maoni yamekubalika na kwa mapenzi ya Mungu, tutafikia makubaliano karibuni ."
Jeshi na Upinzani Waaafikiana Juu ya Kipindi cha Mpito cha Miaka 3 Sudan
0
May 15, 2019
Tags