Kamati ya Maadili ya Bunge Yapendekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele Asimamishwe mikutano mitatu.....Ndugai Awaomba Wabunge Wamsamehe
0
May 23, 2019
Spika Ndugai amependekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele asamehewe
Awali Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23, 2019.
Mbunge Masele akijitetea Bungeni amesema; “Nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa Viongozi wangu wote waliopata usumbufu katika sakata hili akiwemo Rais Magufuli, sikuchonganisha mihimili bali nilikata rufaa baada ya Spika kuniandikia barua ya kunisimamisha bila hata ya kuniuliza lolote”
Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20 mwaka huu akituhumiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba amekuwa na utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili.
Spika Ndugai alilieleza Bunge Mei 16 mwaka huu kwamba kutokana na utovu huo wa nidhamu amesimamisha uwakilishi wa Masele katika Bunge la Afrika (PAP) lililokuwa likiendelea nchini Afrika Kusini na kuagiza mbunge huyo kurejea nchini.
Tags