Katibu Mkuu CCM 'ailipua' UVCCM

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepoteza mwelekeo hivyo kuna kazi ya kufanya kuiweka sawa.

Dkt. Bashiru alitoa kauli hiyo jana  katika mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari jijini Dodoma ambapo alieleza kuwa kwa sasa CCM kinaandaa vyuo vyake vya Ihemi na Zanzibar ili waanze kuwapika vijana kuwa viongozi wazuri.

Alisema vijana wanaotakiwa kupikwa katika vyuo hivyo siyo lazima wawe wana CCM tu bali hata na wengine watapikwa ili wakasaidie maeneo yao. Hata hivyo, katika kipindi cha sasa, atatumia watu mbalimbali atakaowakaribisha ili waweze kuzungumza na vijana hao kuwakumbusha misingi na umuhimu wa jumuiya hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad