KESI ya Katibu Mwenezi wa chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanywa na Rais Magufuli inatarajiwa kuanza kutajwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Wakati akifungua kesi hii Ado Shaibu alisema katiba imeweka masharti maalum ya uteuzi wa mtu wa kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Ibara ya 59 (2) imeweka masharti kuwa mtu anayeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu ni lazima awe mtumishi wa umma mwenye sifa za kuwa wakili kwa miaka 15 mfululizo.
Katika utafiti wake, Ado alisema amebaini kuwa Mwanasheria Mkuu wa sasa, Dk. Kilangi, ana sifa ya kuwa wakili kwa miaka saba tu, ikwa ni chini ya nusu ya miaka iliyowekwa na katiba.
Kesi ya Kupinga Uteuzi wa Rais Magufuli Yaanza Kutajwa Leo
0
May 07, 2019
Tags