Kijana amekamatwa kwa kula bure KFC miaka 2 akidai katumwa kuonja na makao makuu


Mwanafunzi wa miaka 27 anayesoma katika chuo cha UKZN (University Of KwaZulu Natal) amekamatwa na atafikishwa Mahakamani kwa kula bure katika migahawa ya KFC mjini Durban Afrika Kusini akidai kuwa ametumwa kutoka makao makuu kupima ubora wa Chakula.

Kijana huyo amedaiwa kuwa amekuwa na utamaduni wa kuwadanganya wahudumu wa KFC kwa miaka akijidai kuwa ametumwa kuonja ili kubaini chakula hicho, kipo katika viwango vya ubora vinavyotakiwa na makao makuu ya KFC.

Mtandao wa xpouzar.com ambao umeripoti habari hiyo umeeleza kuwa kijana huyo ilikuwa si rahisi kumgundua, ndio maana amefanya tabia hiyo kwa miaka miwili kutokana na uhodari wake wa kuwaadaa wahudumu, kumjua haikuwa rahisi kutokana anakuja na kitambulisho cha mfanyakazi wa KFC kutoka makao makuu akiwa amevaa smart na gari aina ya Limo ambalo rafiki yake alikuwa ni dereva wa muda (Deiwaka).

“Alikuwa akija tulikuwa tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha hatumkwazi, alikuwa tunamuamini kwa sababu alikuwa anajiamini sana hata migahawa jirani ya KFC inamfahamu, akija alikuwa anaelekea moja kwa moja jikoni na kuanza kuangalia kama kila kitu kipo sawa na kuomba sample ya vyakula anavyotaka inawezekana aliwahi kufanya kazi KFC maana anajua kila kitu” alisema moja ya watumish wa KFC
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad