Kijiji Chapiga Marufuku Umbea ....Ukikamatwa Unapiga Umbea Faini Yake ni USD Dola 4 sawa na Tsh. 9200 pamoja na kufanya usafi masaa matatu

Binolonan ambacho ni  Kijiji kinachopatikana kaskazini mwa mji mkuu wa Ufilipino, Manila, kimepiga marufuku kufanya umbea.


Meya wa mji, Ramon Guico, amesema umbea ulisababisha ugomvi mkubwa utokee katika kijiji hicho kitu kilichopelekea vikao vya viongozi kuchukua tahadhari kwa kupiga marufuku kufanya umbea.


Guico alisema kuna umbea wa aina nyingi, lakini katika kijiji hicho kesi nyingi ni za umbea unaohusu mali, pesa na mahusiano. 


Sababu ya marufuku hio ni kukumbusha kwamba kila mtu na hasa wanaoishi katika kijiji hicho anawajibika kwa atakayoyasema. 


Pia wanataka kuonyesha watu wengine kwamba watu wa Binolonan ni watu wazuri na eneo hilo ni salama.


Guico, aliongeza kwamba hatua walizochukua zitaongeza ubora wa kijiji hicho.


Guico aliongeza kwamba maeneo ambayo watu wake hawafanyi umbea yana Baraka zaidi, kwa sababu yeye anaamini watu wana kazi za muhimu zaidi za kufanya badala ya kufanya umbea.


Kwa mujibu wa sheria atakayekutwa na hatia ya kufanya na kueneza umbea na maneno ya uongo atatozwa faini pesa taslimu peso 200 takribni dola za kimarekani 4. Pamoja na tozo hilo la pesa atapewa adhabu ya kukusanya takataka kwa masaa 3.


Atakayekutwa na hatia ya kufanya umbea kwa mara ya pili atatozwa faini ya pesa taslimu peso 1000 takriban dola 20, faini hiyo itaambatana na kupewa adhabu ya kutoa huduma kwa jamii kwa masaa 8.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad